Mark 13:32-37

32 a“Kwa habari ya siku ile na saa hakuna yeyote ajuaye, hata malaika walio mbinguni wala Mwana, ila Baba peke yake. 33Jihadharini! Kesheni! Kwa maana hamjui wakati ule utakapowadia. 34 bNi kama mtu anayesafiri. Anaiacha nyumba yake na kuwaachia watumishi wake kuiangalia, kila mtu na kazi yake, kisha akamwamuru yule bawabu aliye mlangoni akeshe.

35 c“Basi kesheni kwa sababu hamjui ni lini mwenye nyumba atakaporudi: iwapo ni jioni, au ni usiku wa manane, au alfajiri awikapo jogoo, au mapambazuko. 36Kama akija ghafula, asije akawakuta mmelala. 37 dLile ninalowaambia ninyi, nawaambia watu wote: ‘Kesheni!’ ”
Copyright information for SwhKC